DEMU WA CRISTIANO RONALDO APIGWA "KITUMBO" NA MCHEZA FILAMU

KIMWANA mwanamitindo wa Victoria’s Secret, Irina Shayk amenaswa mjamzito na anatarajiwa kujifungua mtoto wake wa kwanza, chanzo kimeliambia jarida la PEOPLE.

Msemaji wa kimwana huyo hajathibitisha ujauzito huo wala kujibu maswali aliyotumiwa na jarida hilo.

Mwanadada huyo ambaye ni rafiki wa kike wa zamani wa nyota wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo, amepewa ujauzito huo na mwigizaji Bradley Cooper, 41.

Shayk, 30, na Cooper wamekuwa katika uhusiano wa kimapenzi tangu mwaka 2015, muda si mrefu sana tangu kimwana huyo alipoachana na Ronaldo na Cooper kumwagana na kimwana wake, Suki Waterhouse.

Wapendanao hao hawafichi kuhusu mapenzi yao na mara kwa mara wamekuwa wakitoka pamoja kuhudhuria hafla mbalimbali.

Licha ya ujauzito, Irina alishiriki kuonyesha mavazi ya Vicroria’s Secret Fashion Show 2016 kwa kupita stejini Jumatano iliyopita.


Ronaldo ameripotiwa kuwa na kimwana mrembo wa Kihispania, Georgina Rodriguez.

No comments