DEPAY, SCHNEIDERLIN RUKSA KUTIMKA MANCHESTER UNITED DIRISHA DOGO


Jose Mourinho hatakuwa na kipingamizi iwapo Memphis Depay au Morgan Schneiderlin atahitaji kuondoka Manchester United na kujiunga na Everton katika dirisha dogo la usajili la mwezi Januari.

Depay na Schneiderlin hawajaanza hata mchezo mmoja wa Premier League msimu huu na hawatarajiwi kujumuishwa katika mchezo dhidi ya  Crystal Palace leo usiku kwenye dimba la  Selhurst Park.

Kocha wa Everton Ronald Koeman ameonyesha utashi wa kutaka kumsajili Schneiderlin, ambaye alifanya nae kazi Southampton.

Aidha, Koeman pia angependa kumsajili  Depay kwa mkopo.

No comments