Habari

DOKII: SIJAACHA KUIGIZA MSINIWEKEE MANENO MDOMONI

on

NYOTA wa filamu za vichekesho, Dokii amefunguka na kusema kuwa pamoja na
kwamba ameokoka lakini hajaacha uigizaji kwa vile anategemea sanaa kupata pesa
za matumizi na za sadaka.
Alisema kuwa kuna watu walimwelewa vibaya aliposema kuwa ameokoka wakadhani
kwamba ameaacha sanaa kumbe si kweli bali anaendelea kuigiza kama kawaida ingawa
ana muda mrefu hajaandaa filamu.
“Nikiacha kuigiza nitapata wapi pesa ya mafuta ya gari, nitapata wapi pesa
ya kula na nitapata wapi sadaka? Watu wasiniwekee maneno mdomoni mimi sijaacha
uigizaji,” alisema Dokii.

Alisema alianza uigizaji mwaka 1999 na alishashiriki filamu zaidi ya 20
ambazo anaamini alizitendea haki hadi kumfanya watu wengi kumfahamu na
kufurahia uigizaji wake wa kuvaa uhusika.

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *