DUDUBAYA: WABAYA WANGU WANAODHANI NIMECHUJA WATASUBIRI SANA

RAPA mkongwe Godfrey Tumaini “Dudubaya” amesema kuwa wabaya wake wanaodhani kwamba amechuja katika muziki watasubiri sana kwavile ana uwezo mkubwa wa kufanya vitu vyake.

Alisema kuwa baada ya kimya cha muda mrefu alirejea kwenye gemu aiwa na wimbo wa “Kokoriko” na sasa amekuja na mwingine uitwao “Inuka” ambao amedai kwamba umekuwa ukitesa kwenye vituo mbalimbali vya radio.

Dudubaya alisema kuwa wimbo huo umemshirikisha msanii T.I.D ambapo anaamini ameutoa wakati mwafaka kutokana na kile alichodai kwamba unazidi kukubalika.


“Ukiona wimbo unachezwa sana kwenye vituo vya radio ujue umekubalika na ndivyo ilivyo kwa “Inuka” ambao kwa kweli ninaamini utafanya vizuri,” alisema Dudubaya.

No comments