GABO ZIGAMBA AWATAKA WASANII WENZAKE KUACHA KUWA NA UMOJA WA "MIDOMONI"

SALIM Ahmed “Gabo Zigamba” amesema bila wasanii kuamua kuwa na ushirikiano wa kweli tasnia ya filamu itaendelea kuyumba na mwishowe kitakachofuata ni kusambaratika.

Alisema, kuwa wapo baadhi ya wasanii ambao wana umoja wa mdomoni huku mioyoni hawao hivyo na kwamba kila mmoja amekuwa akitaka kufanya kazi kivyake.

“Binafsi juhudi zangu ndizo zimenifikisha hapa nilipo hadi mashabiki wakanikubali kwani niligundua kuwa wasanii hatuna ushirikiano wala umoja wa kweli,” alisema Gabo.


Alisema kuwa, njia pekee ya kuendeleza Bongomuvi ni wasanii kujitambua na kutambua thamani yao na kushirikiana badala ya kila mmoja kujiona bora kuliko mwingine, hali ambayo inachangia kuleta utengano.

No comments