GARY CAHILL AIPONDA RAFU YA AGUERO AKIIITA YA “KIUENDAWAZIMU”

BEKI wa Chelsea Gary Cahill ameiita rafu iliyofanywa na straika wa Man City, Sergio Aguero na kusababisha atolewe nje ya uwanja kuwa ni ya kiuwendawazimu.

Katika mchezo wa Jumamosi, Aguero alionyeshwa moja kwa moja kadi nyekundu katika muda wa nyongeza baada ya kumfanyia madhambi David Luiz ambayo ilisababisha kuzuka ghasia zilizosababisha pia kutolewa nje mchezaji mwingine wa Man City, Fernandinho.

Cahill anaelezea kushitushwa na kitendo hicho kilichofanywa na nyota huyo wa timu ya taifa ya Argentina wakati wa mchezo huo ambao Chelsea waliondoka na ushindi wa mabao 3-1 akisema kuwa anavyodhani kitendo hicho kilikuwa si cha kawaida.

“Labda pengine ilikuwa ni hali ya kuchanganyikiwa,” Cahill aliliambia gazeti la The Mirror.

“Alikuwa kama sio yeye, alikuwa tofauti na tabia yake. Ilionekana kuwa rafu mbaya, inashangaza kuona kuwa anafanya hivyo,” aliongeza staa huyo.


Alisema kuwa wakati wa mchezo huo ilikuwa ni vita kati yake na David na kwamba wakati mwingine huchanganyikiwa ndicho kilichosababisha hali hiyo itokee.

No comments