GERARD PIGUE NAE AIPANIA MECHI YA EL CLASICO YA JUMAMOSI HII

BEKI wa timu ya Barcelona, Gerard Pique ni kama kaipania mechi ambayo itawakutanisha na mahasimu wao Real Madrid maarufu kama "El Clasico" baada ya kusema kuwa ni muhimu kwao kuliko wapinzani wao na hivyo wanatakiwa kushinda.

Jumamosi ijayo Real Madrid watasafiri kwenda kwenye uwanja wa Nou Camp wakiwa kileleni mwa michuano ya La Liga kwa zaidi ya pointi sita dhidi ya Barcelona.

Kwa mujibu wa Pique pengo hilo ndilo linaifanya Barca ambao wametoka sare mfululizo kuiona mechi hiyo muhimu mno kwao.

“Ni mechi muhimu kwetu kuliko wao,” alisema nyota huyo kupitia mtandao wa kituo cha mundo Deportivo.

Endapo watashinda watakuwa wakituzidi kwa pointi tisa hivyo itakuwa vigumu kuwafikia,” aliongeza beki huyo.

Jumapili iliyopita Barca walitoka sare ya bao 1-1 dhidi ya Real Sociedad na iliwalazimu kusubiri hadi kipindi cha pili hadi alipofunga staa wao Lionel Messi na kuwawezesha kuondoka na pointi.

Hata hivyo juzi Pique alisema kuwa siku hiyo haikuwa nzuri kwao. Alisema kuwa kwa sasa mambo hayaendi sawa sawa.

No comments