Habari

GONZALO HIGUAIN AMFANANISHA PAULO DYBALA NA LIONEL MESSI

on

STRAIKA
wa Liverpool, Gonzalo Higuain amemfananisha staa mwenzake Paulo Dybala na nyota
wa Barcelona ambaye ni mshindi mara tano wa tuzo ya mchezaji bora wa dunia
“Ballon d’Or” Lionel Messi.
Tangu
mwaka jana Dybala alipowasili Juventus akitokea katika timu ya Pelermo kwa
haraka staa huyo amewezakuonyesha makali yake na kuisaidia timu hiyo kutwaa
mataji ya serea A, Copa Italia na Super Copa Italiana.
Staa
huyo mwenye umri wa miaka 23, raia wa Argentina pia msimu huu ameendelea na
moto huo baada ya kufunga mabao matatu na kutoa pasi zilizozaa mengine mawili
na kuifanya Juve kukaa kileleni mwa Ligi hiyo ya serea A wakiwa mbele kwa
pointi nne.
Kiwango
hicho ndicho kinachoonekana kumkuna raia mwenzake, Higuain ambaye anaamini
Dybala ataweza kufuata nyayo za nahodha wa Argentina, Messi.
“Dybala
na Messi wana mambo mengi yanayofanana. Messi ni bora na amekuwa akionyesha
hivyo kila siku,” alisema Higuain kuuambia mtandao wa Premium Sport.

“Paulo
bado ni mdogo kwani ana miaka 23 ila itategemea na kitakachojitokeza siku za
mbeleni ila ana kila dalili za kuwa mchezaji bora,” aliongeza staa huyo.

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *