GUARDIOLA ASEMA BADO ANAFURAHISHWA NA KIWANGO CHA MANCHESTER CITY

KOCHA Pep Guardiola amesema bado anafurahishwa na kiwango kilichoonyeshwa na Manchester City wakati ilipofungwa na Chelsea na akasema kwamba kilikuwa ni kizuri kuliko walipozifunga Burnley na Crystal Palace.

Rekodi ya Man City kutofungwa ikiwa nyumbani msimu huu kwenye michuano ya Ligi Kuu ilimalizika baada ya kikosi cha Antonio Conte kutoka nyuma kwa bao 1-0 na kisha kikaondoka na ushindi wa mabao 3-1 wakiwa Etihad na huku waliokuwa wenyeji wakimaliza mchezo na wachezaji tisa baada ya Sergio Aguero na Fernandinhokutolewa nje ya uwanja.

“Nilifarijika kuliko ilivyokuwa katika michezo miwili tuliyoshinda. Tulifurahi wakati wa mechi dhidi ya Palace na Brnley kwa sababu tulishinda lakini wakati huo tulikuwa na hofu,” alisema kocha huyo.

“Niliwaeleza wachezaji wangu kwamba vijana mnatakiwa kucheza kama ilivyokuwa mwanzoni mwa msimu. Kuweni huru, onyesheni soka na mmiliki mpira,” aliongeza kocha huyo.


Alisema kuwa kutokana na maagizo hayo anavyodhani kuwa vijana wake waliweza kucheza vizuri.

No comments