HATIMAYE CHELSEA YATHIBITISHA KUMUUZA OSCAR LIGI YA CHINA KWA PAUNI MIL 52


CHELSEA imethibitisha kuwa imemuuza kiungo wake Oscar kwenda Shanghai SIPG kwa pauni milioni 52.

Usajili wa Oscar unakuwa ni ghali zaidi kuwahi kutokea katika klabu hiyo inayoshiriki Ligi Kuu ya China na ataungana na kocha wa zamani wa Chelsea Andre Villas-Boas.

Oscar alishindwa kutamba Stamford Bridge chini ya Antonio Conte akicheza mechi 11 tu msimu huu huku akiwa hajaanza hata mchezo mmoja wa Premier League tangu mwezi Septemba wakati Chelsea ilipofungwa 2-1 na Liverpool.

No comments