HUSSEIN JUMBE ‘KUIBUKIA’ MSONDO NGOMA KESHO MANGO GARDEN


MWIMBAJI na mmiliki wa Talent Band, Hussein Jumbe kesho atakuwa mwanamuziki mwalikwa katika onyesho maalum la Msondo Ngoma litakalofanyika Mango Garden Kinondoni.

Onyesho hilo linalokwenda kwa jina la “Msondo Family Day” litashuhudia mwimbaji huyo mwenye sauti tamu akisalimia kisanii mashabiki kwa kushiriki baadhi ya kazi alizowahi kuzifanya na Msondo Ngoma.

Mmoja wa waratibu onyesho hilo, Abdulfareed Hussein ameiambia Saluti5 kuwa Jumbe tayari amethibitisha kuwa atakuwepo Mango Garden katika “Msondo Family Day”.

No comments