IBRAHIMOVIC APIGA CHAPUO SENTAHAFU VICTOR LINDELOF ASAJILIWE MANCHESTER UNITED


MSHAMBULIAJI mkongwe wa Manchester United Zlatan Ibrahimovic amesema anaamini Msweden mwezake  Victor Lindelof ana kipaji kitakachomwezesha kung'ara Old Trafford.

Lindelof, sentahafu wa Benfica yuko mbioni kusajiliwa na Manchester United dirisha dogo la Januari. 

Ibrahimovic, ambaye magoli yake mawili dhidi ya West Brom Jumamosi iliyopita yamemfanya afikishe magoli 16 kwa United kwenye mashindano yote msimu huu, amempigia chapuo beki huyo mwenye umri wa miaka 22.

"Soka lake linaimarika kwa kiwango cha hali juu. Ni tegemeo kwa timu ya taifa sasa," alisema Ibrahimovic. 

"Anafaa kwa United? Nadhani ameiva yupo tayari kwa klabu yoyote kubwa. Ni juu yake kuchagua nini anataka. Lolote atakaloamua litakuwa jambo jema kwake.

"Najua hayupo sokoni, kwahiyo wacha tumpe nafasi ya kuchagua jambo sahihi".


No comments