IRENE UWOYA ADAI HAPENDI KUTAFUTIWA "KIKI" KINGUVU

MWIGIZAJI wa Bongomuvi, Irene Uwoya hapendi kutafutiwa umaarufu kwa namna yoyote ile kwa madai kwamba jina lake kwenye fani ni kubwa na umaarufu alionao unamtosha.

“Sitaki kiki, sitaki kutafutiwa umaarufu na mtu yeyote kwa sababu jina langu tayari ni kubwa hivyo hao wanaotaka kulazimisha kunitafutia umaarufu wanapoteza muda wao,” alisema Uwoya.

Msanii huyo alisema hayo kufuatia habari za hivi karibuni kwamba anamchukia Wema Sepetu na kufafanua waliosema hayo walimwekea maneno mdomoni wakidhani anahitaji kiki wakati tayari jina lake liko juu.


“Nimepata umaarufu kwenye filamu hadi katika siasa hivyo sihitaji mtu anitafutie umaarufu zaidi ya huo na kama ninautaka nitautafuta mwenyewe na sio kwa njia ya kugombana na wenzangu,” alisema na kusisitiza kuwa jamii inapaswa kuwaunganisha wasanii na si kujaribu kuwagombanisha.

No comments