IRENE UWOYA: WANAODAI NIMWEFULIA WATASEMA MCHANA USIKU WATALALA

NYOTA wa filamu Irene Uwoya amesema kwamba kuna watu wamekua "wakichonga" sana juu yake, lakini yeye hataki kuwajibu kwa kuwa anajua ipo siku watanyamaza.

“Ninajua kwamba watanisema sana na itafika siku watanyamaza ila ukweli utabaki kwamba hawezi kujua maisha yangu na wala sitaishi watakavyo wao bali nitakavyo mwenyewe,” alisema Uwoya.

Alisema kuwa kilichosababisha watu waanze kuchonga juu yake ni kukaa kimya akifanya shughuli zake nyingine tofauti na uigizaji ndipo yakaibuka maneno kwamba kimya hicho kinatokana na kufulia.


Alisema katika maisha yake ni muhimu mtu kujiongeza kuwa na shughuli zaidi ya mmoja kama ambavyo amekuwa akifanya kila siku lakini baadhi ya watu wanamchukulia kama amefulia.

No comments