HATIMAYE iko wazi sasa kuwa mwimbaji na rapa JFour Sukari alikuwa akijidanganya wenyewe pale aliposema hakwenda Dodoma na Twanga Pepeta.

Mapema leo, Saluti5 ilipenyezewa habari za uhakika kuwa JFour yuko safarini na Twanga Pepeta lakini msanii huyo wa TOT Plus alikanusha vikali pale alipopigiwa simu na mtandao huu.

Kinyume na kukanusha kwake, msanii huyu yuko jukwaani na Twanga Pepeta usiku huu huko Dodoma katika onyesho la bendi hiyo linaloendelea katika ukumbi wa Perugina kama anavyoonekana pichani.

Inasemekana Twanga Pepeta imemuazima JFour ili iweze kugawa bendi mara mbili ambapo kundi moja lipo Dodoma na lingine lipo Toroka Uje Tabata jijini Dar es Salaam likisaidiwa Chaz Baba.

Wakati JFour akienda ‘kuokoa’ nyumba jirani, bendi yake ya TOT iko CCM Mwinjuma Mwananyamala usiku huu katika onyesho lao la kila Ijumaa.

Mmoja wa viongozi wa TOT Juma Jerry ameiambia Saluti5 kuwa hawana tatizo na wasanii wao kwenda kupiga ndondo siku ambazo hawana kazi, lakini ni kinyume na utaratibu msanii kuacha show ya bendi yake na kwenda kushiriki onyesho la bendi nyingine …tena bila kuomba ruhusa.

PICHA  NA SHAKOOR JONGO.
USISAHAU KUBONYEZA SUBSCRIBE HAPO
LIKE PAGE YETU YA FACEBOOK Saluti5

Post a Comment

 
Top
Nicolaus Trac