J4 SUKARI SAFARINI DODOMA NA TWANGA PEPETA …TOT kunani!???


ALIYEWAHI kuwa rapa na mwimbaji wa Twanga Pepeta J Four Sukari yuko njiani na bendi hiyo kuelekea mjini Dodoma.

Twanga Pepeta inafanya onyesho mjini humo leo usiku ndani ya ukumbi wa Perugina lakini bado hajajulikana kama J Four atashiriki onyesho hilo au amechukua tu lift ya Twanga kwenda Dodoma kwa mambo yake binafsi.

J Four kwa sasa anaitumikia TOT Plus ambayo alijiunga nayo baada ya kuenguliwa Twanga Pepeta miezi kadhaa iliyopita.

TOT leo usiku itakuwa CCM Mwinjuma Mwananyamala na ni wazi kuwa kutokuwepo kwa J Four kutakuwa ni pengo kubwa kwao.

Mmoja wa mabosi wa TOT Juma Jerry “JJ Mzee wa Mbezi” ameiambia Saluti5 kuwa hana taarifa yoyote ya safari hiyo ya J Four.

Saluti5 ilipomuuliza J Four kwa njia ya simu kulikoni yuko njiani na Twanga Pepeta huku bendi yake (TOT) ikitarajiwa kuwa na onyesho leo usiku, akakanusha vikali.

J Four alisema: “Mimi niko Dar es Salaam na ndiyo kwanza naamka, kama kusafiri kwenda kokote labda nisafiri baada ya onyesho la bendi yangu (TOT) leo usiku”.

Hata hivyo Saluti5 ina uhakika wa asilimia 100 kuwa J Four yuko safarini na Twanga Pepeta. Kitu ambacho Saluti5 haina uhakika nacho ni madhumuni ya safari hiyo.


Meneja wa Twanga Pepeta Hassan Rehani amekataa kusema lolote na kutaka Saluti5 iwasiliane na mkurugenzi wa Aset Asha Baraka. Hata hivyo simu ya Asha Baraka haikupatikana.

Pichani juu ni J Four (kushoto) akiwa na Hosea Bass na nyuma ya bus dogo walilosafiria wanamuziki wa Twanga Pepeta kuelekea Dodoma.

No comments