JADO FFU NA BENDI YAKE MPYA ORIGINAL DAR MUSICA AINGIA STUDIO KUPAKUA NNE MPYA


MWIMBAJI Jado FFU akiwa na bendi yake mpya kabisa Original Dar Musica, ameingia studio kurekodi nyimbo nne kali.

Akizungumza na Saluti5, Jado aliitaja studio hiyo ni On Time Production ya producer Amoroso Soundo.

Nyimbo zinazopikwa studio ni “Hatufanani”, “Ama Zao Ama Zangu”, “Jirekebishe” na “Mtu Box”.

Ukitata kula uhondo wa nyimbo hizo ‘live’ basi fuatana na ratiba ya Original Dar Musica ya wiki hii halafu jichagulie kiwanja kimoja wapo ukawaone.


Jumatano Original Dar Musica itakuwa Friends Corner - Magomeni Kagera, Alhamisi ni New Back in Town – Manzese, Ijumaa watapatikana Mamaland – Ukonga na Jumamosi na Jumapili ni Titanic – Vingunguti.

Ujio huu mpya wa Jado unakuja baada ya kutibuana na mmiliki wa Dar Musica aliyoitumikia tangu alipoondoka Mashujaa Band na ndipo akaibuka na bendi yake mpya - Original Dar Musica.

No comments