JAHAZI MODERN TAARAB WAFANYA SHOO YA "DHARURA" EQUATOR GRILL NA “KUSEBENESHA” MASHABIKI

SAA chache baada ya kuahirisha safari yao ya Morogoro walikokuwa wakashiriki Tamasha la Krismasi, Jahazi Modern Taarab jana waliandaa shoo ndani ya Equator Grill, jijini Dar es Salaam na kupata mwitiko mkubwa wa mashabiki.

Hilo linaendelea kusisitizia kuwa bendi hiyo ambayo hivi sasa iko chini ya Prince Amigo, bado iko juu katika medani ya muziki wa taarab Bongo.


Saluti 5 ilitinga ndani ya ukumbi wa Equator Grill uliopo maeneo ya Mtoni kwa Azizi Ally na kushuhudia “live” namna mambo yalivyokuwa na zifuatazo ni picha sita za wakali hao walivyokuwa wakifanya yao jukwaani.
Waimbaji Fatma Kassim na Mish Mohammed wakiwajibika kwa madoido
Mpapasa kinanda, Mazoea akiwa kazini
 Hapa mcharaza gitaa la solo Emelaa Hemedi akiwa amegeukia u MC
Fatma Kassim akiimba kwa hisia kali
Prince Amigo "akiamsha" kama kawaida yake 
Ally Jay akiwa kazini

No comments