JAHAZI MODERN TAARAB WANOGEWA LEKAM PUB BUGURUNI... sasa ni full raha kila Jumapili


BAADA ya mwishoni mwa wiki kukinukisha Lekam Royal Pub na kupata mwitiko mkubwa wa mashabiki, bendi ya Jahazi Modern Taarab imeamua kuweka ngome ndani ya ukumbi huo ulioko Buguruni Rozana jijini Dar es Salaam.

“Kuanzia sasa tutakuwa tukipatikana hapa kila wiki katika siku za Jumapili, kuanzia majira ya saa 3:30 usiku na kuendelea,” anasema Hamis Boha, mkurugenzi wa bendi hiyo.


Boha amesema kuwa kama ilivyokuwa walipokuwa wakitumbuiza kwenye ukumbi wa Travertine Hotel, Magomeni, watakaohudhuria Lekam pia watafaidi kwa kupata burudani zisizo za kawaida.

No comments