JAHAZI MODERN TAARAB YAENDELEA NA USAJILI …yamnyakua Mosi Suleiman


MWIMBAJI mwenye sauti tamu  na adimu Mosi Suleiman, aliyewahi kung’ara na Zanzibar Stars Modern Taarab na baadae Dar Modern Taarab, amejiunga na Jahazi Modern Taarab.

Mkurugenzi wa Jahazi, Khamis Boha amethibitisha kuwa wamemalizana na Mosi na anaanza kazi mara moja kwenye ofisi yake mpya.

Siku tatu zilizopita, Jahazi ilimrejesha kundini mpiga kinanda maarufu Ally Jay.

Khamis Boha amesema bado Jahazi itaendelea kufanya usajili katika maeneo muhimu yanayohitaji kuongezewa nguvu.
Mosi Suleiman akisaini kujiunga na Jahazi. Kulia ni Khamis Boha mkurugenzi wa Jahazi Modern Taarab


No comments