JAHAZI MODERN TARAB WAPIGA SHOO YA KILO LEKAM ROYAL PUB BUGURUNI… watambulisha nyimbo mpya “Nataka Jibu”

JAHAZI Modern Taarab "Wana wa Nakshi Nakshi", Jumapili usiku waliachia bonge la shoo ndani ya ukumbi wa Lekam Royal Pub, Buguruni na kupagawisha vilivyo mashabiki waliohudhuria.

Shoo hiyo ilizima hisia za kwamba Jahazi Modern inaelekea kufa na badala yake ikathibitisha kuwa bado iko katika nafasi yake na mashabiki wangali wana imani nayo kutokana na jinsi walivyohudhuria kwa wingi.

Muziki mzito uliokuwa unaporomoshwa na wasanii wa bendi hiyo uliwafanya mashabiki wengi waliokuwemo ndani kuvisahau viti kwa muda mrefu na kujikuta wakijimwaga katikati kucheza.


Lakini kibao kipya cha “Nataka Jibu” walichokitambulisha kiliongeza ladha zaidi ya shoo hiyo na kuwacharusha mashabiki waliozidi kumiminika kati na kujirusha kwa raha zao mwanzo mwisho.

PATA PICHA 7 ZA NAMNA MAMBO YALIVYONOGA
 Mwimbaji Mwasiti Kitoronto (kushoto), katika picha ya pamoja na mtangazaji mahiri wa Times Fm, Aisha Mbegu aliyepanda jukwaani baada ya mzuka kumkolea
 Mpapasa kinanda Ally Jay akifanya yake katika kuleta amshaamsha kwa mashabiki
 Mdau wa muziki, Juma Mbizo (kushoto), akifuatilia shoo kwa karibu zaidi sambamba na Aisha Mbegu
 Hapa mwimbaji Mishi Mohammed kama anavyoonekana akiimba kwa mbwembwe za aina yake
 Safu ya waimbaji wa Jahazi Modern wakilishambulia jukwaa 
 Wacheza shoo wa Mashauzi Classic nao walishindwa kuvumilia na kuvamia jukwaa na kutoa burudani ya mwaka
Mwasiti Kitoronto akiimba kwa hisia kali wimbo mpya wa "Nataka Jibu"

No comments