JB ANG'ANG'ANIA MSIMAMO WAKE WA KUSTAAFU KUIGIZA

MKONGWE wa Bongomuvi, Jacob Stephen “JB” ameshikilia msimamo wake wa kustaafu kuigiza licha ya baadhi ya wasanii kumuomba aendelee kushiriki kwenye filamu kwa madai kwamba mchango wake bado unahitajika.

Alisema kuwa ana majukumu mengi ambayo yako mbele yake akiwa na kampuni ya Jerusalem Film hivyo hana budi kupunguza kazi kwa kujikita zaidi katika utayarishaji wa filamu na tamthilia.

“Watu wengi hawajui kile ambacho nimeamua kukifanya, mimi sijatoka katika filamu bali ninataka kuwa mwandaaji na mwongozaji. Bado nitakuwa katika tasnia ya filamu, lakini sio kwa kuigiza,” alisema JB.

Alisemakuwa kwa sasa ana uwezo wa kutayarisha filamu mbili hadi tatu kwa wakati mmoja baada ya kuamua kupunguza majukumu na anaona kwa njia hiyo mambo yatazidi kumwendea vizuri.


Hivi karibuni msanii Chiki Mchoma alisikika akisemakuwa JB hana sababu ya kustaafu kuigiza kwakuwa ni mtu ambaye bado sanaa inamwitaji.

No comments