JEROME BOATENG AMTAKA BOSI WAKE RUMMENIGGE WAKUTANE ANA KWA ANA ILI AMWELEZE KINACHOMSIBU

BEKI ambaye amekaliwa kooni Jerome Boateng amemjibu mkurugenzi mtendaji wa Bayern Munich Karl-heinz Rummenigge akimtaka wakutane binafsi ili amueleze kuhusu tatizo lake binafsi.

Kauli hiyo ya Boateng imekuja baada ya wiki iliyo pita Remmenigge kuhoji kuhusu kiwango kibovu cha nyota huyo mwenye umri wa miaka 28 alichokionyesha katika mchezo ambao walifungwa bila ya kutarajia mabao 3-2 dhidi ya timu ya Rostov katika michuano ya Ligi ya Mabingwa.

Licha ya staa huyo kuwa majeruhi lakini Rummenigge alimtaka Boateng kujirekebisha na kuelekeza nguvu zake katika soka.

Hata hivyo Boateng ambaye alikosa mechi ya Jumamosi ambayo waliondoka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Bayer Leverkusen, anaonekana kubeza kauli ya kigogo huyo mwenye umri wa miaka 61 akimtaka wakutane ili waweze kuzungumza naye.

“Kitu pekee ambacho anaweza kukifanya ni kucheza kuhusu kauli yake,” Boateng aliiambia Sky Sport.

“Wakati mwingine anatakiwa kuzungumza na mimi ana kwa ana ndipo itakuwa vizuri,” aliongeza nyota huyo.


Msimun huu Boateng ameshacheza mechi saba za Ligi ya Bundersilifga na kati ya hizo tano amecheza kikosi cha kwanza na kwa sasa mabingwa hao watetezi wa Ligi hiyo wanashika nafasi ya pili wakiwa nyuma kwa pointi tatu dhidi ya vinara wanaoongoza Ligi hiyo RB Leipzig.

No comments