JOHN TERRY KUWAFUATA FRANK RAMPARD, STEVEN GERRARD

ZAMA na enzi za nahodha wa miaka mingi ndani ya kikosi cha Chelsea, John Terry ni kama vile zinakwenda ukingoni na tayari ameweka Malengo yake mapya.

Malengo aliyonayo sasa ni kwamba mara baada ya kumaliza mkataba wa mwaka moja ndani ya Chelsea anatarajia kufuata nyayo za wakongwe waliotimka katika Ligi za Marekani, China na Japani.

Kauli ya Terry inakuja siku chache baada ya Chelsea kukubali kumuongeza mkataba wa mwaka mmoja wa kukipiga The Bridge.

Kwa kauli hii ni sawa na kusema Terry anafuata nyayo za wakongwe wenzake waliowahi kutamba katika klabu za Chelsea na Liverpool, Frank Lampard na Steven Gerrard ambao wanasakata soka katika Ligi maarufu ya Major League Soccer nchini Marekani.


Hata hivyo tayari Steven Gerrard ameshatangaza kutundika njumu rasmi na kuachana na soka la uwanjani.

No comments