JOSE MOURINHO AANZA MAJIGAMBO MANCHESTER UNITED

KOCHA wa Manchester United, Jose Mourinho ni kama ameanza majigambo baada ya kusema kuwa ilikuwa rahisi kwake kuzoea mazingira ya klabu hiyo.

Bosi huyo wa zamani wa Chelsea alionekana kuwa kikaangoni miezi saba ya kwanza Old Trafford, timu ikishindwa kuwa thabiti na adhabu za FA hivyo kuwasili hatua zake za mwanzo.

Hata hivyo, Mourinho amesisitiza kuwa alijisikia yuko nyumbani mara moja baada ya kujiunga na Man United, jambo ambalo watangulizi wake, David Moyes na van Gaal hawakuthubutu kusema.

“Kwangu mimi ilikuwa rahisi, ni kibarua kigumu lakini rahisi kujisikia nyumbani katika klabu hii. Ni rahisi kuhisi kuwa klabu inahitaji furaha tena,” aliwaambia maripota.

“Nilijisikia vizuri haraka kwa hiyo miezi mitano sita hapa tayari najihisi nipo nyumbani, kwangu mimi ilikuwa rahisi sana.”

“Ni dhahiri kwamba matarajio yapo juu, matokeo bora yanahitajika pia… kupanda kumetufanya tuwe kwenye nafasi ambayo hatukutaka kuwa. Lakini kwa upande wa jitihada na subira ya kazi yangu, subira ya klabu yangu mpya, najisikia furaha sana hapa. Naam.”


Mourinho ameshinda 3-1 dhidi ya Sunderland inayonolewa na bosi wa zamani wa klabu hiyo, David Moyes.

No comments