JOSE MOURINHO SASA ASAKA "UCHAWI" WA ALEX FERGUSON

KOCHA wa Manchester United, Jose Mourinho amefichua siri kuwa amemwomba kocha wa zamani wa timu hiyo, Alex Ferguson kuhudhuria mazoezi ya timu hiyo.

Mourinho alisema ferguson alikubali ombi lake na hivi karibuni alitinga kwenye mazoezi ya timu hiyo.

“Nilitaka wachezaji wamwone huyo gwiji ambaye alileta mafanikio mengi Manchester United, alikuja na tukala nae chakula cha mchana,” alisema Mourinho.


Ferguson ndie kocha mwenye mafanikio makubwa zaidi Manchester United akiwa amesaidia kikosi hicho kutwaa ubingwa mara 13 katika kipindi cha miaka 26.

No comments