JUX ATOA NENO ZITO KUHUSU "TEAM" ZILIZOKO KWENYE MUZIKI... asema zinampandisha msanii lakini pia zinauporomosha muziki

STAA wa muziki wa Kizazi Kipya Juma Jux amefunguka kuhusu timu zilizopo kwenye muziki huo na kusema kuwa zinachafua hali ya hewa mitandaoni kwa kutukana matusi mazito huku baadhi ya wasanii wakikumbana na kashfa.

Msanii huyo anaetamba na wimbo "Wivu" alisema kuwa timu zinasaidia wasanii kufanya vizuri ila hazitakiwi kufika mbali zaidi hadi kutaka kushikana mashati.


“Muziki wetu wakati mwingine unalala sana unatakiwa uchangamke, unajua kunapokuwa na timu hata msanii unayekuwa unashindana naye kazi zinakuwa zinafanyika kwa ubora mtu anakuwa hakuchukulii poa, lakini kitu ambacho sikipendi kwenye hizo timu zisifikie hatua zikaanza kushikana mashati na kuchomana visu,” alisema Jux.

No comments