KAJALA AWATAKA WASICHANA WENZIE KUACHA KUWA "MAGOLIKIPA" NA BADALA YAKE WAJISHUGHULISHE

STAA wa Bongomuvi Kajala Masanja amesema kuwa si vizuri wasichana kutegemea fedha za wanaume kuendeshea maisha na badala yake wanatakiwa kujituma kwa bidii katika kazi.

Alisema kuwa wasichana wengi ambao hawajishughulishi hukaa tu kusubiri wapewe jambo ambalo ni hatari kwa vile vya kupewa vina gharama yake.

“Siyo vizuri wasanii wa kike kama mimi kuamini kwamba hawezi kufanya chochote bila mwanaume bali tunatakiwa kujituma na kutumia fedha zetu wenyewe na siyo kutegemea fedha za wanaume kwani fedha ya mtu inauma,” alisema Kajala.


Alisema kuwa wapo wasanii wengi wa kike akiwemo yeye, wanajituma na wamefanikiwaa hiyo ni ushindi kuwa wanawake wa naweza.

No comments