KAJALA MASANJA AFUNGUKA KUHUSU KURUDIANA NA PETIT MAN

MSANII wa filamu nchini, Kajala Masanja amefunguka juu ya taarifa zilizozagaa kwenye mitandao ya kijamii ya kurudi katika mahusiano yake na aliyekuwa mpenzi wake wa zamani Petit Man.

Mwanadada huyo aliandika hayo kupitia mtandao wa kijamii. “Jamani I think this is too much sasa na mnavuka mipaka. 
Ifike muda watu muwe mnatumia akili kufikiria mnayoyataka kusema. Hivi kama ulishakuwaga na mahusiano na mtu na hayo mahusiano yakaisha so huruhusiwi kuongea nae? Are you guys okay?”


“Hivi mnajua mchango wa Petit katika maisha yangu? Mnajua jinsi alivyonisaidia wakati nipo katika kipindi kigumu cha jela? Au mnakuwa mnaongea tu ili mfurahishe watu… Petit sasa hivi ni part ya familia yangu na sio mambo ya mapenzi. Kwani mimi sijui kama ana mke na ana familia?”

No comments