KIPA HUGO LLORIS AJITIA 'KITANZI' TOTTENHAM HADI MWAKA 2022


NAHODHA wa Tottenham  Hugo Lloris (pichani kushoto) amesaini mkataba mpya wa kuitumikia klabu hiyo ambao utadumu hadi mwaka 2022. 

Kipa huyo No 1 wa Ufaransa amekuwa nguzo ya Tottenham tangu alipojiunga nayo kiangazi cha mwaka 2012 kutoka Lyon kwa ada ya pauni milioni 12.

Na sasa Lloris ameongeza mkataba wake kwa miaka mitano na nusu kwa dili litakalomwingizia pauni 100,000 kwa wiki pamoja na marupurupu kibao.

No comments