KLOPP AMCHANA "LIVE" MAMADOU SAKHO AKIMWAMBIA: "SIKUTAKI!"

KOCHA wa Liverpool, Jurgen Klopp amesema hamtaki Mamadou Sakho.

Sakho hajachezea Liverpool msimu huu licha ya kuwa fiti.
Shirika la soka Ulaya (UEFA), lilimnasa Sakho kwa tuhuma za kutumia dawa za kusisimua misuli zilizokatazwa kwa wanamichezo Aprili, mwaka huu.

Hata hivyo alifutiwa adhabu baada ya kusimamishwa kwa muda


Beki huyo wa zamani wa Paris Saint-Germain alikorofishana na Klopp kwa matatizo ya utovu wa nidhamu na kutimuliwa kwenye kambi ya timu hiyo wakati wa maandalizi ya mwanzo wa msimu nchini Marekani.

No comments