KLOPP ASEMA SASA NI “KUPAKI BASI” KWA KWENDA MBELE

KOCHA wa timu ya Liverpool Jurgen Klopp amesema kuwa wapo tayari kuanza kucheza mpira wa kujihami maarufu kama “kupaki” baada ya kuongeza mechi za kushinda bila kufungwa.

Mabao ya mwisho ya wiki yaliyofungwa na nyota wake Divock Origin na lile la penati lilowekwa kimiani na James Milner ndiyo yaliyowa fanya vijana hao wa Klopp kuondoka na ushindi wa 2-0 dhidi ya Sunderland lakini iliwalazimu kusubili hadi dakika 15 za mwisho za mtanange huo uliopigwa kwenye uwanja wa Anfield.

Wakiwa bado hawaja fungwa katika mechi 14 walizocheza katika mashindamo yote inawafanya Liverpool kuonekana kuwa na mwanzo mzuri msimu huu.

Hata hivyo pamoja na matokeo hayo, Klopp anasema kuwa anavyodhani kwa sasa wanatakiwa kiiga mchezo wa kuegesha basi kama zilivyowafanyia timu mbili walizokutana nazo hivi karibuni.


“Nadhani hakuna wasiwasi timu hii kuanza kucheza kwa kupaki basi, sote tuna uwezo lakini tunahitaji kuwavumilia,” Mjerumani huyo aliviambia vyombo vya habari.

No comments