KOCHA ANTONIO CONTE AKIKUBALI KIWANGO CHA EDEN HAZARD

KOCHA wa Chelsea, Antonio Conte ni kama amekikubali kiwango cha straika wake Eden Hazard, baada ya kusema kuwa hashangazwi na uchezaji wake.

Straika huyo raia wa Ubelgiji alionyesha kiwango kibovu msimu wa 2015/16 ikiwa ni baada ya kutangazwa mchezaji bora wa Ligi Kuu England.

Hata hivyo msimu huu Hazard amerejea kwenye ubora wake na majuzi alikuwa miongoni mwa waliofunga mabao 3-1 dhidi ya Bournemouth na kuifanya Chelsea ifikishe michezo 12 bila kufungwa.

Kutokana na ushindi huo, Conte alimsifia straika huyo mwenye miaka 25 kwa kufunga mabao tisa na kutoa pasi zilizozaa mabao katika michezo 17.

“Namfahamu Eden wakati wakiwa wapinzani wetu katika timu ya taifa na kiukweli nilikuwa nikimwangalia mara kwa mara kwenye televisheni,” alisema Conte.

“Sishangazwi nae kwasababu ana kipaji cha hali ya juu,” aliongeza Mwitaliano huyo.

Alisema kuwa hata hivyo cha muhimu ni kuwa amekuwa akikitumia kipaji chake kuisaidia timu na akasema kuwa anachoshangaa ni jinsi nyota huyo anavyojituma uwanjani akiwa na mpira na hata asipokuwa na mpira.


Kwa sasa Chelsea wapo mbele kwa pointi saba kileleni na Jumamosi watakuwa wakiikaribisha Stoke.    

No comments