KOCHA ANTONIO CONTE AWATAKA VIJANA WAKE KUKAZA MSULI ZAIDI

KWA kile ambacho unaweza kusema ni kama hajaridhika licha ya Chelsea kuendeleza wimbi la ushindi baada ya hivi karibuni kuondoka na mabao 3-1 dhidi ya Bournemouth wakiwa kwenye uwanja wa nyumbani wa Stanford Bridge, kocha Antonio Conte amewataka wachezaji wake kukaza buti zaidi ili waendelee kushinda.

Katika mchezo huo, vinara hao wa Ligi Kuu walikuwa hawana mshambuliaji wao mahiri, Diego Costa na kiungo mkabaji N’Golo Kante kutokana na kuwa wamefungiwa, lakini Pedro akatupia mawili huku eden hazard akifikisha bao lake la 50 katika michuano ya Ligi hiyo na kuifanya klabu yao iweke rekodi ya ucheza michezo 12 bila kufungwa.

Hata hivyo pamoja na rekodi hiyo, Muitaliano huyo alisema kuwa bado ana kiu ya kutaka kushinda michezo mingine mingi zaidi.

“Tulicheza vizuri na tungeweza kufunga mabao mengi zaidi, lakini nimefurahishwa na kiwango cha wachezaji walichokionyesha,” alisema Conte katika mahojiano ya BBC Sport.

“Tumecheza bila wachezaji wetu wawili muhimu lakini nadhani tumecheza vizuri,” aliongeza kocha huyo.

Alisema kwamba kushinda mechi 12 mfululizo katika Ligi hiyo sio jambo rahisi na kwamba pamoja na kuwa ni jambo la ajabu lakini bado anataka waendelee kushinda.


Alisema siku nne zijazo watakuwa na mechi nyingine ngumu lakini akasema kuwa watajiandaa vyema kutokana na kuwa kila timu inapania kuwafunga.

No comments