KOCHA SWANSEA LAWAMANI KWA KUFUNDISHA KIZAMANI NA KUKOSA UBUNIFU

KOCHA wa Swansea City, Bon Bradley amelaumiwa kwa kufundisha mazoezi ya kizamani na kukosa ubunifu.

Nyota wa Swansea wana mashaka na uwezo wa kocha huyo kama ataweza kuiokoa kutoshuka Ligi Kuu England.

Bladley aliajiriwa kufundisha kikosi hicho pamoja na kuwa alikuwa hana uzoefu wa kufundisha klabu yoyote barani Ulaya.

Watu ndani ya klabu hiyo wamemlalamikia kwa kukosa mbinu za kisasa.


Uzoefu wa Bladley wa kimataifa ni wa kuzinoa timu za Misri na Marekani tu. 

No comments