KOCHA WA STOKE CITY ASEMA ANAAMINI LIVERPOOL INAWEZA KUTWAA UBINGWA

KOCHA wa Stoke City, Mark Hughes amesema kwamba anavyoamini Liverpool wanaweza kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu England, lakini akawatahadharisha akisema inaweza kuwawia vigumu kama ukame wa taji hilo utawaandama kwa muda mrefu.

Kikosi cha Jurgen Klopp hadi mapema majuzi kilikuwa nyuma dhidi ya Chelsea lakini kilikuwa na mechi moja mkononi kabla ya kuivaa Stoke juzi hiyohiyo.

Kikosi hicho pia hakijawahi kutwaa ubingwa tangu mwaka 1990 ambao ulikuwa ni wa 18 tangu kianze kushiriki michuano hiyo.

Kutokana na hali hiyo, Hughes ambaye aliwahi kutwaa mataji mawili ya Ligi Kuu akiwa mchezaji wa Manchester United alisema juzi kuwa itakuwa ni kazi kubwa kumaliza ukame huo.

“Kila mwaka unakuwa mgumu zaidi, kila mwaka utazidi kuwa mgumu,” alisema kocha huyo.


Alisema kwamba wakati akichezea Man United alikuwa akizungumza hivyo mwanzoni, katikati na mwishoni mwa msimu.

No comments