Habari

KOCHA WEST BROM AKIMWAGIA SIFA KIKOSI CHA ARSENE WENGER… asema ni kizuri kuliko cha Chelsea

on

KOCHA
wa timu West Brom, Tony Pulis amekisifia kikosi cha Arsenal akisema kuwa ni
kizuri kuliko cha vinara wa Ligi Kuu England, Chelsea.
Kauli
hiyo imekuja baada ya bao lililofungwa na straika Olivier Giroud dakika za
mwisho za mchezo ambao Arsenal walikilaza kikosi hicho cha Pulis kwa bao 1-0
wakiwa kwenye uwanja wao wa Emirates.
West
Brom vilevile mwezi huu walifungwa dakika za mwisho wakiwa kwenye uwanja wa
Stanford Bridge na kuifanya Chelsea ifikishe mechi ya 12 katika michuano ya
Ligi Kuu.
Hata
hivyo licha ya kikosi hicho cha Antonio Conte kuwa mbele kwa pointi saba dhidi
ya Arsenal, Pulis anaamini kuwa Arsene Wenger ndiye ana kikosi imara.
“Kama
utaangalia wachezaji ambao hawakucheza leo (majuzi), na ambao hawakuwemo
kikosini na ukiangalia Chelsea nadhani Arsenal ndio wana kikosi imara,” alisema
kocha huyo.
“Muda
wote wanakuwa na kasi na inakuwa vizuri kuwaangalia kama Chelsea watafanya nini
kipindi watakapokutana nao,” aliongeza kocha huyo.

Pulis
alisema kuwa pamoja na Chelsea wapo kileleni mwa Ligi Kuu itawalazimu kuongeza
wachezaji wengine mwezi ujao.

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *