KOCHA ZIDANE AKATAA ALVARO MORATA KUUZWA KWA DAU LOLOTE

KOCHA wa klabu ya Real Madrid, Zinedine Zidane amekanusha juu ya tetesi za usajili wa nyota wake, Alvaro Morata na kuzipasha timu zinazomwania kwa kuwaambia hawana mpango wa kumuuza kwa gharama yoyote.

Kabla ya kauli ya kocha huyo, Morata alivumishwa kutakiwa na Manchester United ambao wanapambana kwa ajili ya kuimarisha kikosi cha mzunguuko wa pili wa Ligi ya premier.

Kocha wa mashetani hao Jose Mourinho amekuwa akimzungumzia Morata kama sehemu ya mkakati wake wakukisuka kikosi cha kusaka heshima na ubingwa katika duru la pili.

Lakini ukweli uliopo juu ya hatua ya Real Madrid kuachana na mpango wa kumuuza kiungo huyo utakatisha matumaini ya kumnasa nyota huyo.

Kocha Zidane amenukuliwa na Sky Sport kuwa klabu yake haina mpango wa kuuuza kiungo huyo licha ya kupokea ofa kutoka katika timu mbalimbali ikiwemo Man United.

Mara baada ya taarifa za kiungo huyo kuamua kutua Old Trafford, kocha Zidane ameachana na mpango wake huo na kutangaza rasmi kutouzwa kwa Morata.


Morata mwenye umri wa miaka 23 alijiunga tena na mabingwa hao wa Ligi ya Mabingwa msimu akitokea Juventus alikokwenda kucheza kwa dau la pauni mil 23.

No comments