Habari

“KUNA KITU CHA KUONGEZA HAPA ARSENAL” ASEMA KOCHA ARSENE WENGER

on

KOCHA
Arsene Wenger ni kama kabaini upungufu katika kikosi chake cha Arsenal baada ya
kusema kuwa kinahitaji kitu maalum cha kuongeza baada ya Olivier Gioroud
kufunga bao dakika za mwisho lililofanya iondoke na ushindi mwembamba wa bao
1-0 dhidi ya West Brom.
Katika
mchezo huo wa majuzi uliopigwa kwenye uwanja wa Emirates, Gunners walikizidi
nguvu kikosi cha Tony Pulis lakini ukuta wa Baggies ukawa imara.
Hata
hivyo Arsenal ambao walikuwa wameshapoteza mechi mbili za Ligi Kuu kwa kufungwa
mabao 2-1, baadae walifanikiwa kupata bao kupitia kwa Giroud zikiwa zimebaki
dakika nne baada ya kuunganisha mpira uliopigwa na Mesut Ozil.
“Mwisho
wa yote tulitakiwa kuwa wavumilivu kutokana na kuwa tulikuwa tukicheza na
kikosi cha West Brom ambacho kilikuwa kimejipanga,” Wenger aliwaambia waandishi
wa habari.
“Walikuwa
wamejipanga vizuri ili wasifanye makosa katika safu ya ulinzi na kama
walivyofanya isingekuwa rahisi kuwafunga,” aliongeza kocha huyo.

Alisema
kuwa walipata nafasi nyingi na kupiga mashuti mengi lakini bado kuna kitu
maalum.

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *