KUZOMEWA KWA FELLAINE NA MASHABIKI KWAWACHUKIZA MASTAA MAN UNITED

NYOTA wa Manchester United wamechukizwa na kitendo cha kiungo wa timu hiyo, Marouane Fellaine kuzomewa.

Fellaine analaumiwa kwa kusababisha penati iliyosaidia Everton kusawazisha bao dhidi ya Manchester United hivi karibuni.

Mashabiki wa Manchester United walimzomea wakati alipoingizwa kipindi cha pili cha mechi dhidi ya Tottenham wikiendi iliyopita.


Beki wa Manchester United Phil Jones alisema wachezaji hawakufurahishwa na kitendo cha Fellaine kuzomewa kwa kueleza wanaamini hakutendewa haki.

No comments