LADY JAYDEE: SIWEZI KUANZISHA "LEBO" KWA KUFUATA MKUMBO

MKONGWE wa muziki wa Kizazi Kipya Lady Jay Dee amesema kuwa katika maisha yake huwa hafanyi mambo kwa kufuata mkumbo na kwamba hawezi kuanzisha lebo ya kurekodi muziki kwa vile wasanii wengi wanafanya hivyo.

Nyota huyo alitaja baadhi ya mambo ambayo hahitaji kuyafanya kwa kufuata mkumbo kuwa ni kuanzisha lebo ya kurekodi muziki kwa vile kuna wasanii mwengi wanaofanya hivyo.

“Wasanii wengi wanaanzisha lebo za kurekodi muziki kwa vile wenzao wamefanya hivyo hivyo lazima kila mtu awe na lebo, kila mmoja wetu ana njia yake ya kufanya kazi sitaki kufuata mkumbo,” alisema Jay Dee.


Msanii huyo pia alisema kuwa siyo vizuri wasanii wachanga kukimbilia kuomba kubebwa na wasanii majina makubwa badala yake wanaonyesha vipaji vyao kwanza ndipo waweze kusaidiwa iliwasonge mbele.

No comments