LIVERPOOL WAWATEMBELEA WAGONJWA NA KUWAFARIJI KRISMASI HII

JURGEN Klopp na wachezaji wake wa Liverpool wametumia muda wao katikati ya ratiba ngumu za mechi kwa ajili ya kuwatembelea na kuwafariji wenye mahitaji.

Liverpool walitembelea hospitali ya watoto ya Albel Hey na kufurahia fursa ya kuweka tabasamu katika nyuso za watoto hao juzi Ijumaa.

Klopp, Jordan Henderson, Adam Lalana, Dejan Roviren, Divock Oriji na Daniel Sturrige wote walipigwa picha wakiwapa watoto hao zawadi ya Krismasi mjini Liverpool.

Watoto katika hospitali hiyo walipata fursa ya kukutana na kupiga picha na nyota hao wa soka kuelekea Sikukuu ya Krismasi.

Henderson alipiga picha akiwa na mtoto aliyekuwa amevalia jezi ya Barcelona huku mtoto huyo mgonjwa akionekana kufurahia kukutana na nahodha huyo wa Liverpool.

Liverpool kwa sasa wanashika nafasi ya pili katika msimamo wa Ligi Kuu England wakiwa na pointi 37, sita nyuma ya vinara Chelsea kuelekea mechi zao za kesho katika Boxing Day.


Liverpool itaivaa Stoke kwenye uwanja wa Anfield hiyo kesho.

No comments