LOTHAR MATTHAUS ASEMA PIERRE-EMERICK AUBAMEYANG NI BORA KULIKO PAUL POBGA


Lothar Matthaus ametoa tathimini inayoonyesha kuwa mshambuliaji wa Borussia Dortmund  Pierre-Emerick Aubameyang ni bora kuliko kiungo wa Manchester United Paul Pobga. 

Nyota huyo wa zamani wa Ujerumani aliyeshinda Kombe la Dunia mwaka 1990 amesema Aubameyang ndiye angestahili kuvunja rekodi ya uhamisho na si Pobga.

Pogba alirejea United kutoka Juventus kiangazi kilichopita kwa ada ya pauni milioni 100.

"Iwapo mchezaji kama Pobga ananunuliwa kwa euro milioni 105, basi  Borussia Dortmund ingepata euro milioni 150 kwa  Aubameyang," alisema Matthaus na kuongeza kuwa: "Aubameyang anaweza kuleta utofauti kwenye mchezo lakini Pobga hawezi".
Lothar Matthaus


No comments