LUCAS VAZQUEZ ACHEKELEA JAMES RODRIGUEZ KUBAKI REAL MADRID

STRAIKA wa Real Madrid, Lucas Vazquez amefurahia kuona staa mwenzake, James Rodriguez akibaki kwenye klabu hiyo.

Awali staa huyo wa timu ya taifa ya Colombia alikuwa akihusishwa sana kuwa ataitema klabu hiyo ya Santiago
Bernabeu baada ya mwezi huu kukiri akisema kuwa kukosa nafasi ya kucheza mara kwa mara itamlazimu kufanya uamuzi mwingine.

Chesea ilikuwa ikiripotiwa kuwa miongoni mwa klabu ambazo zinafukuzia saini yake, lakini juzi wakala James Jorge Mendes akasema kuwa ataondoka kabla ya msimu huu kumalizika.

“Ni rafiki yangu mkubwa na nina matumaini atabaki. Nina imani kubwa sana kwake na ninavyodhani ni mchezaji mzuri,” alisema straika huyo.


Mchezaji mwingine wa Real Madrid ambaye amekuwa akitajwa kuwa ataondoka mwakani ni Pepe ambaye anasemekana kupata ofa kubwa kutoka nchini China baada ya mkataba wake kumalizika Juni mwakani.

No comments