Habari

LUKE SHAW KAZI NAYO KWA MOURINHO …nafasi yake yazibwa ipasavyo na Daley Blind na Matteo Darmian

on

Luke Shaw ana kazi kubwa ya kumshawishi   Jose Mourinho kwamba bado anahitajika Manchester United baada ya kuwa na msimu mbovu chini ya kocha huyo Mreno. 

Maumivu yamemfanya beki huyo wa kushoto wa England akose michezo mitano tangu alipotolewa kwenye mchezo wa FL Cup dhidi ya West Ham mwezi uliopita.

United imeshinda mechi nne kati ya hizo na kutoa sare moja, imeruhusu magoli mawili tu na kutoa picha kuwa Mourinho sasa ameipatia ‘fomula’.

Phil Jones na Marcos Rojo wameng’ara kwenye beki ya kati na kufukia mapengo ya Chris Smalling na Eric Bailly huku Daley Blind na Matteo Darmian wakimudu vizuri nafasi ya Luke Shaw.

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *