LULU AWAWEKA MKAO WA KULA MASHABIKI WAKE MWAKA 2017

MWIGIZAJI wa Bongomuvi, Elizabeth Michael “Lulu” amewataka mashabiki wake wajiandae kumshuhudia akifanya vitu vyake mwaka ujao kwa kuwa 2016 alikuwa bize na masomo.

“Mwaka 2016 haukuwa mwaka wangu wa kazi ndio maana sikufanikiwa kushiriki kwenye tuzo kwa sababu nilitingwa na masomo lakini 2017 nitakuwa nje ya masomo hivyo wajiandae kushudia kazi zangu nyingi,” alisema Lulu.

Alisema kuwa mshika mbili moja humponyoka, ndio maana aliamua kuelekeza nguvu kwenye masomo kwanza na baadae arudi katika fani kama kawaida, hivyo mashabiki wakwe atawapa vitu wanavyovitaka.


Amesema kwamba kipindi chote ambacho amekaa nje ya tasnia hiyo amepata muda wa kutosha wa kuangalia soko la filamu likoje na sasa ataibuka kwa kishindo akiwa na kazi zitakazoendelea kumweka juu.

No comments