MABOSI MANCHESTER UNITED WASEMA “TUNA IMANI NA MOURINHO”

INASHANGAZA lakini ndio ukweli wenyewe wale waliokuwa wanadhani kuwa kocha wa Manchester United Jose Mourinho anatengeneza njia ya kulalia kuti kavu uwanja wa Old Trafford kutokana na matokeo yasiyoridhisha ya timu hiyo wamebugi.

Kocha huyo Mreno ni kama vile ana mganga bab kubwa kwani pamoja na matokeo mabaya ya timu ya Ligi Kuu England matajiri wa klabu hiyo wamesema bosi huyo aliyejipa jina la utani Specil One anafanya kazi nzuri na wana imani naye.

Matajiri hao wamekwenda mbali zaidi kiasi hata cha kusema Manchester United ya sasa chini ya Mourinho ni timu kuliko ile ya wakati wa kocha Luis Van Gaal.

Rokedi kati ya Mourinho na Van Gaal katika vipindi vinavyofanana na hadi kufikia sasa msimu huu na uliopita zinaacha pengo linaloonyesha Van Gaal alifanya vizuri zaidi kuliko mrithi wake.

Lakini pamoja na takwimu kutodanganya kati ya wawili hao bado wamiliki wa timu hiyo wanampa shavu Mourinho kama mtu sahihi kuijenga United itakayofikia kiwango cha kocha Alex Ferguson.

Kauli ya matajiri hao kuwa matokeo mazuri siyo jambo la maana sana kwa sasa bali muhimu ni kujenga timu inamtia jeuri Mourinho.

United ilikumbana na wakati mwingine mgumu kwenye mechi za Ligi Kuu za Ligi Kuu England baada ya mwishoni mwa wiki iliyopita kulazimisha sare ya bao 1-1 dhidi ya Evrton.

Baada ya sare hiyo shutuma tele zilielekezwa kwa Mourinho kuhusiana na utetezi mbovu wa kikosi chake.


“Ushindani wa sasa Ligi haitoi nafasi kwa timu isiyo na uwezo kushika nafasi ya sita kama ilivyo kwetu,” alisema Mourinho.

No comments