MALAIKA AJITETEA KUHUSU KASHFA YA KUWEKWA KINYUMBA KWA KIVULI CHA SHOO MAREKANI

WAKATI ikidaiwa kwenye mitandao ya kijamii kwamba Malaika yuko Marekani kwa ufadhili wa yule pedezyee aliyemtorosha Linah huko kwa miezi kibao chini ya kivuli cha "ziara ya muziki", mwimbaji huyo wa kibao cha "Rarua" amefafanua kuhusu ziara yake hiyo itakayomalizika Februari mwakani.

Malaika amesema hatua ya kurefusha ziara yake ya maonyesho nchini Marekani ni dalili tosha kwamba muziki anaoufanya unazidi kukubalika.

Alisema kuwa baada ya kufika nchini humo mwezi uliopita alipata nafasi ya kuwa mgeni mwalikwa kwenye maonyesho la kundi la Sauti Sol la Kenya na kuonyesha vitu vyake.


“Baada ya hapo nilipata mialiko mingi ambayo imenifanya niongeze maonyesho zaidi hadi Februari mwaka ujao kwani ilikuwa nirudi mwezi huu wa Desemba,” alisema Malaika kwa njia ya mtandao na kuongeza.

"Msanii kama mimi kukubalika huku ni bahati kwangu, hivyo sina budi kujisifu na hiyo inanipa ari ya kuendelea kuandaa kazi nyingi zaidi ili kupanua wigo wa soko la nyimbo zangu." 

No comments