MANCHESTER UNITED KUMFUNGIA KAZI ANTONIE GRIEZMANN WA ATLETICO MADRID


MANCHESTER UNITED inaagalia uwezekano kumpata mshambuliaji wa Atletico Madrid Antoine Griezmann ikiwa ni dalili kuwa kocha Jose Mourinho anataka kuboresha safu yake ya ushambuliji.

Licha ya Atletico Madrid kuwa na msimu mbovu, lakini makali ya  Griezmann mwenye umri wa miaka 25 yanaendelea kuonekana ambapo tayari ameshafunga mabao tisa na kupika mengine sita kwenye michuano yote.

Suala kumpata dirisha la Januari linaonekana gumu, lakini uwezekano wa kufanya biashara majira ya kiangazi ni mkubwa ingawa United watalazimika kulipa zaidi ya pauni milioni 60.

Kama United itafanikiwa kumnasa nyota huyo wa kimataifa wa Ufaransa, basi ataungana na  swahiba wake mkubwa Paul Pobga.

No comments