MANCHESTER UNITED, LIVERPOOL ZAINGIA VITANI KUMWANIA KIUNGO ANDRE GOMES WA BARCELONA

KIUNGO imara wa Barcelona Andre Gomes ameziingiza vitani klabu za Primiuer ikiwemo Manchester United Tottenham na Liverpool.

Magazeti ya nchini Hispania yameripoti juu ya raia huyo wa Ureno kutakiwa na klabu zote mbili huku kila moja ikidai kufanya mazungumzo ya awali.

Kiungo huyo ambaye pia ni tegemeo katika kikosi cha taifa cha Ureno amekuwa akihusishwa na tetesi za awali za kujiunga na mabingwa wa England Lecester City.

Lakini hata hivyo taarifa za hivi karibuni zimebainika kuwa Gomes amekuwa na mchango mkubwa katika ushindi wa timu yake ya Valencia huku akipiga pasi za mwisho zilizozaa mabao katika mechi 41 alizopangwa.


Jarida la Marca la mwishoni mwa juma lililopita liliripoti kuwa Liverpool inamuhitaji Games kwenye umri wa miaka 22 kama kiungo atakayerejesha uimara wa safu ya kiungo kwa ajili ya msimu ujao.

No comments